
Mume wa
mwanamke wa nchini Pakistan aliyepigwa mawe hadi kufa Farzana Parveen,
kwa kukataa kushiriki katika mipango ya ndoa na mwanaume aliyechaguliwa
na familia yake amesema kuwa alimuua mke wake wa kwanza ili aweze
kufunga ndoa na ParveenMwanaume huyo Mohammad Iqbal,
amesema kuwa
alitaka kuwasilisha maombi yake kwa Parveen hivyo aliamua kumuua mke
wake kwanza ambapo mamlaka za nchini Pakistan zimesema mke huyo wa
kwanza aliuwawa miaka sita iliyopita.Alikamatwa na polisi na baadae
kuachiwa kwa dhamana kwasababu mtoto wake wa kiume alimsamehe kutokana
na kitendo hicho.
Mtoto
wake wa kiume ambaye kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 20
amethibitisha taarifa hizo na kusema baba yake alitumikia kifungo cha
mwaka mmoja gerezani.
Parveen
ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu alipigwa mawe hadi kufa na
kundi la watu wakiwemo kaka zake, baba yake na ndugu wa familia yake
Mashariki mwa mji wa Lahore ambapo waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif
amemtaka waziri wa Jimbo hilo kuwasilisha maelezo juu ya tukio hilo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment