STAA wa
sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman ameonesha upande wake
wa pili baada ya kuwabwatukia wakwe zake aliposikia kuwa wana mpango wa
kumpa talaka ili aachane na mumewe Sunday Demonte kutokana na tabia yake
kwa kuwa siyo mwanamke wa kuoa (wife material).
Akizungumza
na mwanahabari wetu juzikati jijini Dar, Aunt alidai kuwa alikerwa na
jambo hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na kuwawakia kuwa hajaolewa
na ndugu hivyo mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba, amekuwa akisikia mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na mumewe.
Alidai
naye ni binadamu hivyo jambo hilo limekuwa likimkera kwa sababu
wanaongea maneno hayo pembeni na kwamba hakuna hata mmoja aliyewahi
kumfuata na kumwambia juu ya suala hilo, zaidi amekuwa akiambiwa na watu
wengine tu.
Akifafanua
zaidi, Aunt alisema kwamba anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa Demonte
kuendelea kumtolea maneno ya kejeli kila kukicha na wakati kama
wanahisi kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza kumtafuta na
kuzungumza naye.
Alitiririka
kuwa jambo ambalo halimpendezi ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu
kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka kumpatia talaka.
“Ujue
hao ndugu wanaotaka kunipa talaka wanatakiwa waelewe kuwa mimi
sijaolewa na wao, hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo lao, maana
niko vizuri na mume wangu, wala hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana
ishu za kupeana talaka,” alisema Aunt.
Ndoa
ya Aunt imekuwa ikisengenywa tangu ilipofungwa mwezi June, 2012 kufutia
staa huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye inasemekana anaishi Dubai.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment