MBALI ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na
makampuni ya kutengeneza pombe kutoa tahadhari kuwa unywaji wa pombe
kupita kiasi ni hatari kwa afya, ‘janki’ Geoffrey Mlelwa (26), mkazi wa
Ipogolo mjini hapa, amejikuta akiyakatisha maisha yake kwa kudaiwa
kugida pombe kupindukia.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri juzikati ambapo kijana huyo
alikuwa katika Soko Kuu la Manispaa ya Iringa akiwa na wenzake wakipiga
ulabu kwa staili ya kuchanganya (kuchoma sindano) ndipo Geoffrey
alipopitiliza na kusababisha apoteze uhai.
Wakizungunza na mwanahabari wetu, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa kijana huyo enzi za uhai wake alikuwa ni mtu wa kunywa pombe za kienyeji aina ya ulanzi na bangi ila siku hiyo alionekana mwenye ‘mihela’ hivyo kuachana na kunywa pombe aliyoizoea na kuanza kunywa pombe ya kisasa kama grants, viroba na kuchanganya na ulanzi ndani ya chupa moja.
“Mbali ya ‘kuchanganya madawa’, kijana huyo hakula chakula chochote tangu alipoanza ‘kupiga vyombo’ na alipozidiwa, rafiki yake alimkokota na kumpeleka chumbani kwao (geto) kabla ya asubuhi kuamka na kumkuta amekufa,” alisema shuhuda mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Alisema kuwa kwa kawaida kijana wake anamtambua kama ni mlevi wa pombe na mtumiaji wa madawa ya kulevya na kuwa hata katika chumba chake walimkutana na chupa ambayo ndani yake ilikuwa imechanganywa pombe mbalimbali.
Alisema anaamini kuwa mchanganyiko huo wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya ndivyo vilisababisha kifo hicho hivyo kuwashauri vijana kuachana na matumizi ya pombe kupita kiasi na madawa ya kulevya kwani wakiendelea kilichomuua mwenzao ndicho kitakachowaua.
>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment