Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
vuguvugu la kutaka mapadri wa Kanisa Katoliki duniani waoe limezidi kukua kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa hilo nao kupendekeza watumishi hao waoe kama wanaume wengine.Waumini hao walisema mara nyingi wamekuwa wakisikia baadhi ya mapadri wamezaa au wana mademu, kwa hiyo hawaoni sababu ya kuendelea kuwazuia kuoa.
Papa francisco
“Kama padri ana demu au amemjaza mwanamke mimba hadi amezaa, sasa kwa nini wasiruhusiwe kuoa kuliko kutenda dhambi? Waoe tu,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Simon Andrew, mkazi wa Mwenge jijini Dar.
Hilo limekuja kufuatia hivi karibuni kanisa hilo kuandikiwa barua ya kutaka
waruhusu mapadri waoe.


Barua hiyo inadaiwa kutoka katika kundi moja la wanawake 26 kutoka nchini Italia walio na hamasa za mapenzi na mapadri wa kanisa hilo kubwa duniani.
Barua hiyo ilidaiwa kutumwa kwa Papa Francis ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa hilo ulimwenguni.
Katika barua hiyo, wanawake hao walisema wamekuwa wakitaka kushiriki katika
uhusiano wa kimapenzi na mapadri
hao lakini kikwazo ni sheria hiyo.


Juzi, mwandishi wetu alikwenda Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kukutana na Katibu wa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo, Denis Aminias na kuzungumza naye kuhusu watu kutaka mapadri waoe  ambapo alisema:

“Kwanza wale wanawake (wa Italia) walikosea kupeleka malalamiko kule (kwa Papa). Suala la matamanio lipo katika maisha yetu ya ubinadamu.
“Sisi kama kanisa tutaendelea kusimamia katika misingi ileile ya kutooa.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top