Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This




Wapiganaji wa Al Shabaab wametimuliwa kutoka Mogadishu ingawa hufanya mashambulizi ya kuvizia
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab limeshambulia bunge la Somalia na kusababisha vifo vya watu kadhaa mjini Mogadishu.
Milipuko na milio ya risasi imesikika huku bunge likishambuliwa, wabunge wakiwa ndani kwa mkutano.

Gari lililokuwa na mabomu lilipuka leo kabla ya saa sita mchana na kufuatiwa na milipuko mingine pamoja na milio ya risasi.

Wabunge pamoja na wafanyakazi wengine waliweza kuokolewa punde baada ya gari kulipuka.
Mashambulizi hayo bado yanaendelea huku wapiganaji hao walifyatua risasi wakiwa ndani ya msikiti mmoja karibu majengo ya bunge.
'Bunge la Somalia'

Wabunge wawili wameuawa chini ya mwezi mmoja
Bunge la kwanza rasmi la Somalia lilianza kufanya kazi miaka miwili iliyopita tangu Somalia kutumbukia katika vita mwaka 1992.

Serikali ya Somalia imekuwa ikiendesha vita dhidi ya kundi la kiisilamu la al-Shabab ambalo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011.
Bunge hilo, ambalo huendesha vikao vyake mjini Mogadishu limewahi kushambuliwa ikiwemo mwaka 2009 na 2010.

Mwezi jana Mbunge mmoja aliuawa kwa kulipuliwa huku mwingine akipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi mawili tofauti.
Wanajeshi 22,000 walio chini ya muungano wa Afrika wanasaidia vikosi vya Somalia kupambana na Al Shabaab.

Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti mkubwa wa miji kadhaa nchini Somalia, bado linadhibiti maeneo mengi ya vijijini.
Chanzo bbcswahili 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top