Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Dr. Dre yupo njiani kuwa rapper wa kwanza
BILLIONAIRE pale kampuni ya Apple itakapoinunua
kampuni yake yake Beats Electronics.
Kwa mujibu wa TMZ, Apple inadaiwa itainunua
Beats kwa gharama ya $3.2 BILLION. Dre na
mwanzilishi wa Interscope, Jimmy Iovine ndio
walioanzisha kampuni hiyo. Dre na Jimmy
walianzisha kampuni hiyo mwaka 2008 kwa
kutengeneza headphone lakini sasa wanatengeneza
pia spika, vifaa vya sauti vya kwenye magari na
mtandao wa kustream muziki.

Deal hiyo inaweza kukamilika wiki ijayo na itakuwa
deal kubwa zaidi ya kampuni Apple. Dre alikamata
nafasi ya pili kwenye orodha ya Forbes ya wasanii
wa hip hop matajiri zaidi akiwa na $550 million
nyuma ya Diddy mwenye $700 million.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top