Shambulio Khost, Afghanistan
Waandishi
wawili wa habari wanawake wa kigeni wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu
mmoja aliyekuwa amevalia sare za polisi mashariki mwa Afghanistan.
Habari kutoka Afghanistan zinasema mmoja wa wanawake hao alifariki dunia, na mwingine alijeruhiwa vibaya.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Khost karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan.
Tukio
hilo limekuja wakati Afghanistan ikiimarisha ulinzi kabla ya kufanyika
uchaguzi wa rais Jumamosi ikiwa ni kukabiliana na vurugu za wapiganaji
wa Taliban.
Rais mpya
atamrithi rais wa sasa Hamid Karzai, ambaye amekuwa madarakani tangu
mwaka 2001 ulipoangushwa utawala wa Taliban, lakini kikatiba anazuiwa
kugombea kipindi cha tatu cha uongozi.
"Waandishi
wa habari wawili wanawake wameuawa kwa kupigwa risasi asubuhi leo ndani
ya eneo la makao makuu ya polisi, ambapo wengine wamejeruhiwa vibaya,"
msemaji wa jimbo la Khost Mobarez Mohammad Zadran ameliambia shirika la
habari la Ufaransa, AFP.
Amesema kuwa mtu huyo mwenye silaha alikuwa amevalia sare za polisi.
Kundi la Taliban limeongeza mashambulio katika wiki za hivi karibuni, ili kuharibu maandalizi ya uchaguzi.
Mwezi
uliopita mwandishi wa habari mwandamizi wa shirika la Agence
France-Presse, Sardar Ahmad, aliuawa pamoja na watu wengine nane, wakati
wapiganaji wa Taliban waliposhambulia hoteli moja ambayo hukaliwa na
raia wengi wa kigeni mjini Kabul, Afghanistan.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment