Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mtalii mmoja mwenye jinsia ya kike ambaye ni raia kutoka nchini Uingereza amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kugundulika akiwa amejichora 'Tattoo' ya Budhaa kwenye mkono wake.



Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Naomi Michelle Coleman, alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona 'Tattoo' hiyo kwenye mkono wake wa kulia.

Budhaa alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.

Msemaji wa polisi alisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini.

Hakimu aliamuru Bi Coleman arejeshwe nchini mwao.

Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao.

Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.

Bi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa punde ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa, walimkamata.

Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top