
Adhabu ya kiboko kwa wanafunzi imeharamishwa katika shule zote nchini Kenya
Wazazi katika kaunti ya
Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya
mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.
Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Hata hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.
Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.
Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile
wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo
walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha
kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini
Kenya.
Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment