STAA wa filamu za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, amewataka kina dada wanaomtaka mahusiano ya kimapenzi kukaa mbali naye, kwani kwa sasa ameamua kutulia na mpenzi wake, na anatarajia kufunga ndoa.
Kupitia
ukurasa wake wa facebook, PHD aliandika kuwa kwa sasa yupo tayari
kumweka hadharani mpenzi wake, ambaye anatarajia kufunga naye ndoa hivi
karibuni, hivyo hataki kufuatwa na wasichana ambao hawapendi maendeleo
yake.
“Nimekuwa
nikisumbuliwa sana kwa kipindi kirefu, hata mimi pia nimewachezea sana
watoto wa watu, sasa nimeamua kutulia na kuwa mwanaume bora, maana
nimegundua nilikuwa nafanya ujinga, umri ushaenda, natakiwa niwe na
familia yangu,” aliandika.
Mbali
na hilo, PHD alisema yupo katika hatua za mwisho za maandalizi ya video
ya ngoma yake mpya anayotarajia kuisambaza mwezi huu inayojulikana kwa
jina la ‘On My Wedding Day’.
Alisema
katika wimbo huo, amezungumzia mambo mengi ambayo anatarajia yatakuwepo
siku yake ya harusi, hivyo anaomba sapoti kwa mashabiki ili iweze
kufanya vizuri.
PHD
ni kati ya nyota wa Bongo wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu na
muziki, kutokana na ubora wa kazi zake na anavyoweza kucheza uhalisia
mbele ya kamera.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment