![]() |
| Ndugu jamaa na marafiki wa Sunday Mwambelo wakimjulia hali katika hospitali ya rufaa Mbeya alikolazwa baada ya kucharangwa mapanga na bosi wake aliyefahamika kwa jina la Simon Njangaje |
![]() |
| Sunday Mwambelo akijuliwa hali na dada yake Never Mwambinga katika hospitali ya Rufaa Mbeya alikolazwa baada ya kucharangwa mapanga na bosi wake |
WAKAZI
wa kitongoji cha Sae Jijini Mbeya hivi karibuni walimuokoa na kifo
mfanyabiashara wa bucha katika buncha ya Simon Butchery iliyopo Sae
Jijini Mbeya, Sunday Mwambelo ambaye alifungiwa katika bucha na
kucharangwa mapanga na watu wawili waliofahamika kwa majina ya Simon
Njangale na Daud Edson.
Hatua
hiyo ilifuatia tukio la kutisha ambalo lilikuwa linaendelea katika moja
ya vyumba vya bucha la nyama ambapo watu watatu walifika eneo hilo
majira ya saa 1:00 jioni na kuufunga mlango wa bucha hiyo kwa nje kisha
wakaanza kumcharaza mapanga muuza nyama huyo.
Ilidaiwa
kuwa mara baada ya watu hao kuingia katika bucha hilo walizima mshumaa
ambapo mmoja wao alibaki mlangoni na wawili kati yao waliingia buchani
na kuchukua panga na shoka kisha kuanza kumuadhibu Sunday ambaye ndiye
muuzaji wa nyama katika bucha hiyo.
Mashuhuda
wa tukio hilo walidai kuwa mmoja kati ya watu hao ndiye mmiliki wa
bucha hiyo na kuwa walifikia hatua hiyo baada ya mfanyakazi wa buchani
hapo kuingiza hasara ya sh.25,000 ambazo ni sehemu ya fedha za mauzo ya
siku hiyo.
Kwa
mujibu wa Mwambelo ambaye amedumu katika biashara hiyo kwa zaidi ya
miaka 10 ni kwamba mara baada ya kuulizwa kuhusu hasara ya kiasi hicho
cha fedha alimwambia tajiri yake kuwa atafidia hasara hiyo kesho yake
jambo ambalo tajiri wake hakukubaliana nalo na hivyo kuchukua uamuzi wa
kumkata kwa mapanga na kusababisha damu nyingi kumwagika buchani.
''Ghafla
walianza kunikata kata kwa mapanga, nikaishiwa nguvu nikakaa chini huku
damu zikinivuja, wasamaria wema waliingia kuniokoa,'' alisema Mwambelo
kwa taabu kutokana na maumivu aliyonayo.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa baada ya kusikia purukushani
katika bucha hiyo waliamua kusogea na kuona dalili za mtu kupigwa ndipo
walipoingia na kumuokoa kijana huyo na baadaye kuwapeleka kituo cha
polisi huku majeruhi akikimbizwa hospitali.
''Wananchi
walifika na kumuokoa Sunday wakaanza kuwapa kipigo wale jamaa,
wakawachukua hadi kituo cha Polisi cha Kati na jamaa wakawekwa
ndani,''alisema dada wa majeruhi Never Mwambinga.
Never
alisema kuwa jamaa hao walidhamiria kumuua nduguyake kwani hatua ya
kumcharanga kwa mapanga huku wakiwa wamezima mshumaa na kufunga mlango
ilikuwa inaashiria dhamira mbaya.
Aidha
Jeshi la Polisi kupitia kwa mmoja wa Ofisa wa ambaye kutokana na
taratibu za Jeshi hilo sio msemaji wa Polisi alisema kuwa watu wawili
ambao ni Simon Njangale mmiliki wa bucha na mtu mmoja Daud Edson
wanashikiliwa kufuatia tukio hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea kwa
ajili ya kuwafikisha mahakamani.
CHANZO MKWINDA BLOG
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro














Post a Comment
Post a Comment