Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kamanda Ahmed Msangi.
Mkazi wa kijiji cha Itimba wilayani Mbeya, Happy Petter (16) anashikiliwa na polisi kwa kumpiga mtoto wa kufikia na kumsababishia kifo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi mtoto huyo Francis Maneno (2) alifariki dunia wakati akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya.
Kamanda Msangi alisema Francis alifikishwa hospitalini hapo akitokea kijijini kwao Itimba kutokana na majeraha aliyokuwa nayo mwilini yaliyosababishwa na kipigo alichokipata kutoka kwa mama yake wa kambo.
Alisema  Aprili 4  saa 2:00 asubuhi mama huyo alimpiga mtoto sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha ambapo chanzo cha kipigo hicho hakijafahamika.
Katika tukio jingine mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Chapwa katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi Blanda Charles (9) amekufa baada ya kuzama katika mto Chapwa wakati akiogelea.
Alisema mwili wa mwanafunzi huyo uligunduliwa na mmoja wa wapita njia, Kapanda Chisunga alipokuwa akivuka mto huo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top