![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/11/140411121346_implant_labgrown_vagina_624x351_wakeforestinstitute_nocredit.jpg)
Ni mara ya kwanza kwa uke wa mwanamke kukuzwa katika maabara
Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote
inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio,
kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote
wakati wa tendo la ndoa.
Wataalamu walisema kuwa utafiti wao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.
Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu ya utumbo inatumika.
Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.
Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment