Mama yake huwa anamuandalia kuku kama
chakula cha siku lakini anakataa na kutaka
apewe vipande vya matofali.
Kwa siku moja anakula vipande kadhaa vya
matofali ambapo kwa makadirio huwa
anakula kilo 3 kila siku.
Fundi huyo wa kujenga nyumba Pakkirappa
Hunagundi anasema kwamba ameanza kula
vitu kama hivyo tangu akiwa na miaka 10 na
anaweza kukosa chakula lakini hawezi
kukosa kula vipande vya matofali.
Akiwa anapata chakula chake hicho
akipendacho(matofali) huwa anahitaji
kikombe cha maji tu ili kushushia na
mwenyewe anasisitiza kwamba hajisikii
tofauti kabisa.
Mkazi huyo wa kijiji cha Karnataka nchini
India anasema anataka kuzunguka India
nzima akionyesha watu uwezo wake huo na
kujipatia pesa kwa kuonyesha maajabu hayo.
KUTANA NA MTU WA AJABU,CHAKULA CHAKE NI TOFALI PEKEE.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment