Sheikh Abubakari shariff (makaburi)
Mhubiri
aliyedaiwa kueneza itikadi kali za kiisilamu nchini Kenya Abubakar
Shariff Ahmed anayejulikana kwa jina lengine kama Makaburi, ameuawa.
Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa ambako alikuwa anaishi.
Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi kwa kueneza itikadi kali za
kiisilamu miongoni mwa vijana wa kiisilamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya
na kuchochea vitendo vya kigaidi.
Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kuenda kupigania kundi la
wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Makaburi amekuwa
akiyakanusha.
Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu katika msikiti wa Majengo, Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri huyo mwenye utata.
Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika msikiti Musa ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata ikitakadi kali za kiisilamu.
Haijulikani ni nani aliyemuua Makaburi.
<<<<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZAIDI>>>>>

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment