Waziri mkuu wa Ubelgiji ni kiongozi wa pili Ulaya kutangaza kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja
Waziri mkuu wa Ubelgiji anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja, Elio Di
Rupo amewasomea viongozi wa Afrika na kuwataka kuheshimu haki za watu
wanaotengwa ikiwemo wapenzi wa jinsia moja.
Alisema ni jambo la kushangaza na lisilokubalika kwamba watu wanahukumiwa kwa sababu ya wanavyochagua kuishi maisha yao.
Bwana Di Rupo alikuwa anahutubia kongamano la viongozi wa Afrika na
Muungano wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji lililohudhuriwa na Marais wa
Afrika.
Mwaka huu Nigeria na Uganda zilikaza sheria zake kuhusu mapenzi ya jinsia moja.
Nchini Uganda yeyote anayepatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja watafungwa maisha jela
Wanaharakati wanaopinga mapenzi ya jinsia moja Uganda
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vimeharamishwa katika nchi
nyingi za Afrika ambako mapenzi ya jinsia moja yanaonekana kama kitendo
kiovu na kisichokubalika.
Bwana Di Rupo ni afisa wa pili wa ngazi ya
juu Ulaya kutangaza kuwa yeye ni shoga. Waziri mkuu wa Ieceland Johanna
Sigurdardottir pia amejitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
"hatuwezi kukubali kuwa baadhi yetu wananyimwa haki zao na kuchukuliwa
hatua za kisheria kwa kuwa wapenzi wa jinsia moja,'' alisema waziri mkuu
huyo
Rais Museveni na mwenzake wa Nigeria Goodluck Jonathan hawajajibu kisomo hicho.
Maafisa wakuu wa Uganda wamekuwa wakitetea msimamo wa Rais Museveni
kuhusu sheria yake kali ya mapenzi ya jinsia moja wakisema kuwa Uganda
ni nchi huru ambayo mataifa ya magharibi hayawezi kuishawishi hivi hivi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment