Matokeo ya awali kwa baadhi ya vituo
yanaonesha kuwa mgombea wa CCM
Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa asilimia
90.
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la
Chalinze yametangazwa Chama cha
Mapinduzi CCM kimepata jumla ya kura
20812,na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA),kimepata idadi ya
jumla kura 2828 na chama cha Wananchi
CUF kimepata kura 474.
Hivyo chama cha Mapinduzi CCM
kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la
Chalinze
CCM 20812 CDM 2638 CUF 473 AFP
78 NRA 59.
Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Chalinze
umefanyika huku ukigubikwa na kasoro
kadhaa, ikiwa ni pamoja na watu wachache
kujitokeza vituoni kupiga kura, wapiga kura
kulalamika ‘kupokwa’ vitambulisho vyao,
vituo kuwa majumbani kwa watu, huku pia
kukiwa na hofu ya vurugu.
Aidha Wananchi wa Chalinze walikuwa
wakipiga kura mbunge wao, kuziba nafasi
iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo, Said Bwanamdogo aliyefariki
mapema mwaka huu.
BREAKING NEWS:-Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda Kiti cha Ubunge Jimbo la Chalinze kura 20812 dhidi kura 2638 za CHADEMA.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment