Wanawake wanaochelewa kuzaa
wanakabiliwa na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi. Huu sio
utafititi tu balo maoni ya daktari mmoja mkuu mjini Nairobi Kenya.
Athari za kuchelewa huko ni pamoja na kukumbwa
na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na matiti pamoja na
matatizo wakati wa kujifungua.Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi.
Mtaalamu wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa mtoto wao wa kwanza hii ni hatari kubwa.''
Bwana Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.
Fibroids zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
Wanaochelewa kuzaa pia wanakabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hatari hizi ni nyingi tu, sasa chaguo ni kwako.
>>>bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment