TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ETINA SILUMBA (44) MKAZI WA MPEMBA
WILAYA YA MOMBA AMEMUUA MUME WAKE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MISHECK
MWASHIUYA (52) M
KAZI
WA MPEMBA WILAYA YA MOMBA KWA KUMKATA KISOGONI NA KICHWANI NA KITU
KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA NA KISHA KUMVUNJA SHINGO NA MGUU WA
KUSHOTO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA
21:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA IPAPA, KATA YA IPUNGA, TARAFA YA VWAWA,
WILAYA YA MBOZI. UCHUNGUZI UNAONYESHA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA
KIMAPENZI. MTUHUMIWA KABLA YA KUTENDA TUKIO HILO INADAIWA KULIKUWA NA
UGOMVI KATI YAKE NA MAREHEMU. MTUHUMIWA AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO ILI
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIMAPENZI KWA NJIA YA KUKAA
MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA WATU WANNE KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA KUISHA.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA
MAJINA YA 1. ULILE ERASTO (30) 2. ERNEST MJEMBE (40) 3. HAMIS
MWANYOMBOLE (28) NA 4. HALIDI SAULI (33) WOTE WAKAZI WA SOWETO JIJI NA
MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAFANYABIASHARA YA KUUZA POMBE BAADA YA MUDA
KUISHA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA MAJIRA YA SAA 01:15 USIKU WA KUAMKIA
TAREHE 12.03.2014 KATIKA ENEO LA MAMA JOHN, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA
IYUNGA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUFUATA NA KUZINGATIA TARATIBU ZA
KUENDESHA/KUFANYA BIASHARA ZAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA
KUJITOKEZA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment