TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
- MTU MMOJA AUAWA KWA TUHUMA ZA WIZI WILAYA MBOZI.
- MWANAMKE ATUPA MTOTO WA SIKU MOJA CHOONI BAADA YA KUJIFUNGUA.
- MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI KUMI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NOEL MWAMBENE (38) MKAZI WA KIJIJI CHA
SUMBALUELA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KATWA SEHEMU MBALIMBALI ZA
MWILI WAKE KWA KUTUMIA MAPANGA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI
KATIKA KIJIJI CHA HASANGA, KATA YA VWAWA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA
MBOZI BAADA YA WATU HAO KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NI MWIZI.
AIDHA, INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA MHALIFU MZOEFU NA ALIKUWA ANATAFUTWA KWA TUHUMA MBALIMBALI ZA MAKOSA YA UVUNJAJI.
MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBOZI. JUHUDI ZA
KUWATAFUTA WALE WOTE WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE
WATUHUMIWA WANAO WAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA
KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO PILI:
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWACHANE AMAN (18) MKAZI WA IDWELI
ALIJIFUNGUA MTOTO JINSI YA KIKE NA KUMTUMBUKIZA KWENYE SHIMO LA CHOO CHA
ENELI SAMOJA ROZINA AKIWA HAI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.03.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA
KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE. MTOTO HUYO ALIYEKUWA NA UMRI WA SIKU MOJA ALIOPOLEWA AKIWA
TAYARI AMEFARIKI DUNIA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. CHANZO CHA TUKIO HILI
KINACHUNGUZWA NA WAKATI HUO HUO UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILI
UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUTUPA WATOTO KWANI NI
KINYUME CHA MAADILI NA MWENENDO MWEMA WA JAMII, PIA NI KINYUME CHA
SHERIA ZA NCHI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO
MDOGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BEATRICE SWALO MWENYE UMRI WA MWAKA
MMOJA NA MIEZI KUMI AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI WAKATI ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA ZAHANATI YA RUANDA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE NDOO YA MAJI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 12:45 MCHANA HUKO
MAKUNGURU, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA BAADA
YA MAREHEMU KUTAMBAA NA KUELEKEA KWENYE NDOO ILIYOKUWA NA MAJI NA KISHA
KUTUMBUKIA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO
ALIKUWA KAZINI NA MTOTO ALIKUWA NA MSICHANA WA KAZI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO IKIWA
NI PAMOJA NA KUWEKA MBALI VITU VYA HATARI KAMA VISU, VIDONGE NA VITU
VINGINE VYA HATARI KWA WATOTO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment