Mtoto Said Siraji(13), mkazi Majengo Kaskazini wilayani
Kahama mkoani Shinyanga aliyedaiwa kukakatwa shingo na baba yake usiku wa
kuamkia Machi nne mwaka huu, amefariki dunia leo
mchana katika Hospitali ya
Rufaa ya Bugando mjini Mwanza.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazin Noel Makula
Mseven amesema Marehemu Siraji aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika Shule ya
Msingiya Majengo amefariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi
mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa Siraji Mariamu Idd awali
alieleza, siku ya tukio Marehemu Siraji alichukuliwa na baba yake mzazi
anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa
wazazi hao walikwishaachana siku nyingi
Alfajiri ya Machi nne Salvatory
ambaye kwa sasa yuko Rumande alimchukua Siraji na kumpeleka kwenye makaburi ya
majengo kwa nia ya kumchinja lakini hakufanikiwa kumuua huku akimwachia jeraha
likimwaga damu nyingi kabla hajaokotwa na wasamaria na kupelekwa hospitalini.
Museven amesema Julai mwaka jana Salvatory alitaka
kumchinja mke wake Mariam lakini akaokolewa na Mseven kitu kilichomuuzi
salvatory na kutaka kumchinja mwenyekiti huo wa kitongoji tuhuma iliyompeleka
gerzani kwa kipindi cha miaka miwili..
Hata hivyo mseven amesema siku amemwokoa mariam Salvatory
alitaka kumchinja mtoto wa jirani ili kutimiza azma yake ikashidikana hali
inayodhaniwa sasa imekamilika baada ya kumchinja mtoto wake Marehem Siraj
Habari ambazo hazijathibitishwa na idara ya upelelezi
wilayani humo zimesema, Salvatory amewaeleza maafisa wa polisi kwamba kitendo
hicho amekifanya kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason na kwamba alitaka
kuchangia damu ya mtoto mdogo akakataliwa.
Mauaji haya yametokea kwa wakati jamii ya wana kahama inakabiliwa na balaa la kuamini vitu na mambo yasiyo na msingi kama lile la kubaini wachawi na imani ya Freemason ambayo haijulikani hata ilikotoka wala msingi wake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment