Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Geoffrey Mutai bingwa wa mbio za Kilomita 21 za New York
Bingwa Mtetezi wa mbio za New York Marathon Geoffrey Mutai alitoka nyuma na kuthibitisha udedea wake katika barabara za mji huo wa Marekani alipokata utepe akitumia muda wa saa moja na sekunde hamsini.

Muingereza Mo Farah, hata hivyo, ndiye aliyewaduwaza mashabiki wake nchini Marekani alipokunguwaa na kuanguka baada ya takriban kilomita tisa na kisha akajifua na kurejea kwa kishindombio zikikaribia kukamilika .
Bingwa huyo wa mbio za mita elfu tano na mita elfu kumi za olimpiki alimaliza katika nafasi ya pili sekunde 18 pekee nyuma ya Mkenya mshikilizi wa muda bora katika mbio za marathon duniani.
Farah alishikwa na kisunzi punde baada ya kukamilisha mbio hizo na alilazimika kubebwa kwa machela.
Mo Farah azirahi baada ya kukamilisha mbio za New York
Muingereza huyo baadaye alisema alikuwa sawa na kuwa ataendelea na mazoezi yake kabla ya kushiriki mbio zake za kwanza za marathon katika mashindano ya London Marathon zitakazoandaliwa mwezi ujao.

Mkenya mwengine Stephen Sambu alimaliza katika nafasi ya tatu sekunde moja pekee nyuma ya Mo .

Ilikuwa siku njema kwa wakenya kwani Sally Kipyego vilevile kutoka Kenya alitwaa ubingwa wa kitengo cha wanawake akisajili muda wa saa moja dakika 8 na sekunde 31.

Muda huo ndio wa kasi zaidi katika kitengo hicho cha wanawake.
Bizunesh Deba, kutoka Ethiopia alimaliza wapili huku Mmarekani Molly Huddle akikamilisha orodha ya tatu bora.
Wanariadha 20,000 walistahimili kiwango cha nyuzijoto zaidi ya 30 na kushiriki mbio hizo za kilometer 21 .

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top