MKAZI wa kitongoji cha Sogea katika Mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba, Pendo Lyala (18) amejifungua mtoto katika choo cha nyumba ya kulala wageni. Pendo alijifungua Machi 10 mwaka huu saa 4:00 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Kiswahili , iliyopo nyuma ya Shule ya Msingi Mwaka, mkabala na barabara kuu iendayo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mmoja
wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni aliyekuwa zamu, Tresia
Albeto, alidai msichana huyo aliingia usiku huo na mpenzi wake
aliyejiandikisha kitabuni kwa jina la Fred Gamba, mkazi wa Njombe,
ambaye alikuwa amechukua chumba namba tano.
Tresia
alidai mara baada ya kuoneshwa chumba hicho, Gamba alitoka nje na
kuingia katika chumba hicho mara tatu katika nyakati tofauti, akiwa
anamuacha mpenzi wake ndani na kuna wakati aliingia akiwa na mfuko wa
plastiki (Rambo) uliokuwa na chipsi na soda.
Mhudumu
huyo alisema baada ya Gamba kutoka mara ya mwisho na kwenda nje,
ilisikika sauti ya kike ikiomba msaada, jambo lililomsukuma kwenda
kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.Alidai baada ya kuingia katika chumba
hicho, alimkuta mwanamke huyo akiendelea kupiga kelele ya kuomba msaada
akiwa katika choo cha chumba hicho.
Alidai
alikwenda moja kwa moja chooni, kulikokuwa kukitokea sauti na kumkuta
msichana huyo amelala chini na mtoto aliyekuwa amejifungua muda mfupi,
alikuwa pembeni ya shimo la choo akilia.
Alidai
kuwa kutokana na mayowe yaliyopigwa na mwanamke huyo, baadhi ya wageni
waliokuwa katika nyumba hiyo, pia waliamka na kujaribu kutoa huduma ya
kwanza, lakini walikwama kwa sababu ya ukosefu wa vifaa salama.
Tresia
alidai hali hiyo iliwachanganya kwa kutokujua la kufanya hadi
alipojitokeza msamaria, ambaye ni miongoni mwa wapangaji aliyekuwa na
mke wake, alipomchukua na kumpeleka katika Kituo cha Afya Tunduma.
Akizungumzia
tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii katika mamlaka ya Mji mdogo wa
Tunduma, Godfrey Simbeye alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa
msichana huyo anaendelea kupata matibabu hospitalini hapo na hali ya
mtoto inaendelea vizuri.
Simbeye
alidai msichana huyo alikuwa na Gamba ambaye walikutana naye usiku huo
na kwamba alipokuwa chumbani, alihisi haja kubwa ndipo alipoenda chooni
na wakati huohuo kujisikia uchungu.
Akizungumza
katika wadi ya wazazi, Pendo alidai alishangaa kuona mtoto, kwani
hakujua kama muda wa kujifungua ulikuwa umefika. Alidai kuwa Gamba
walikutana kwa usiku huo na kufanya makubaliano.
Pendo
alidai kuwa ni mhudumu katika baa aliyoitaja kwa jina la Udizungwa,
iliyopo eneo la ofisi za CCM Kata ya Tunduma, ambako ndiko alikutana na
Gamba.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment