Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema hana mpango wa kuwahoji Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na chama hicho kwa sababu ya misimamo yao inayokinzana na miongozo ya chama, kwa kuwa anawafahamu wote kwa majina na idadi yao haizidi kumi.
Kauli hiyo ya Kinana inafuatia taarifa
zilizoripotiwa na gazeti hili hivi karibuni kuwa, CCM kimeanza kuwahoji
baadhi ya wabunge wake, ambao ni Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kwa
sababu ya kupingana na maelekezo ya chama hicho kuhusu Muundo wa
Serikali mbili.
“Sisi (CCM) hatuhoji mtu kwa sababu ya kuwa na
msimamo tofauti, kwani hawa wenye msimamo tofauti na chama hawazidi kumi
ama siyo zaidi ya 15,” alisema Kinana na kuongeza;
“Hawa watu mimi nawajua kwa majina, mmoja (jina
tunalo) ni hatari zaidi kwa sababu anaweza kuwakusanya wengine na
kuwashawishi wafuate msimamo wake, lakini waliobaki wote, hawatishi kwa
kuwa wanabaki na misimamo yao wenyewe.”
Kwa mujibu wa habari hiyo, wajumbe waliohojiwa ni
wale wanaotokana na Ubunge wa Jamhuri ya Muungano na ambao wanataka
Muundo wa Serikali tatu. “Ni kweli hata mimi niliitwa na akaniambia
(mwakilishi wa chama) ametumwa aniletee ujumbe kuwa niko kwenye orodha
ya watu 90 na nikiendelea na msimamo wangu nitachukuliwa hatua,”
alieleza mmoja wa wajumbe waliodai kuwa wamehojiwa na Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM.
Maelezo ya Kinana
Kinana aliliambia gazeti hili kuwa, kulingana na
muundo wa chama hicho tawala, viongozi wanaoweza kuwahoji watu ni yeye
Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti, Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri
Mkuu na Mwenyekiti wa chama Taifa. “Tena tunafanya hivyo kwenye vikao
maalumu na kwa sababu ambazo haziwezi kuwa siri.”
Kinana alieleza kuwa taarifa kwamba CCM imewahoji
watu 90 kutokana na kuwa na misimamo tofauti na chama hicho kuhusu
Serikali mbili na kura ya wazi, siyo za kweli na anaamini imesambazwa na
watu kwa malengo yao binafsi. Kinana anafafanua kuwa CCM kama chama
kikubwa nchini chenye wafuasi karibu nchi nzima, hakiwezi kudhibiti
mitizamo ya watu na kimsingi tofauti za mitazamo ndiyo msingi wa
demokrasia.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment