Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), David Misime - SACP
Bangi zilizokamatwa katika msako huo uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Dodoma
Zana za kuvunjia zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma baada ya msako mkali
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu nane (8) waliokamatwa
wakiwa na kilo moja na misokoto 104 ya bangi, zana za kuvunjia yakiwemo
mapanga, mikasi, visu, nondo pamoja na mirungi gramu 500.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME - SACP amesema mafanikio haya yametokana na msako unaoendelea
Mkoani Dodoma wa kupambana na wahalifu na uhalifu uliofanyika eneo la
Chang’ombe tarehe 11/03/2014 majira ya saa 01:00Hrs hadi 05:00Hrs na
ulihusisha zaidi kero za uvutaji wa bangi na kupelekea kufanya uhalifu
katika maeneo mbalimbali manispaa ya Dodoma.
Kamanda MISIME amewataja waliokamatwa katika msako huo kuwa ni:-
1. HALFANI S/O MUHEZA mwenye miaka 25, Mgogo, Mkulima.
2. STEWART S/O SYLVESTER mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima.
3. SHABAN S/O IBRAHIM mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima.
4. ABDALLAH S/O IDDI mwenye miaka 18, Mnyaturu, Mkulima.
5. FIKIRI S/O JONAS mwenye miaka 20, Mgogo Mkulima.
6. ALLY S/O NURU mwenye miaka 30, Mgogo, Mkulima
7. SAIMON S/O ZABRON mwenye miaka 43, Mchaga, Mkulima.
8. ALBERT S/O CHARLES mwenye miaka 18, Mgogo, Mkulima wote wakazi wa eneo la Chang’ombe, Manispaa ya Dodoma.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kesho tarehe 12/03/2014 kujibu tuhuma zao zinazowakabili.
Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kumtafuta Dereva wa gari
linalosemekana kuwa ni TOYOTA LAND CRUISER GX STANDARD rangi nyeupe
baada ya kumgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la JULIAS S/O
SANDUKU mwenye miaka 50, Mkaguru, Mkulima, Mkazi wa Gairo katika eneo la
Kijiji cha Visimi Kibaigwa na kumsababishia kifo mpanda baiskeli huyo.
Kamanda
MISIME amesema dereva huyo ambaye alikuwa anatokea Dodoma kuelekea
uelekeo wa Mkoa jirani wa Morogoro baada ya kumgonga mpanda baiskeli
huyo, alishuka kutoka ndani ya gari na kumwangalia aliyemgonga
alipogundua amefariki akageuza gari kurudi njia ya Dodoma na kuwaambia
wananchi waliojitokeza kuwa anaenda kutoa taarifa Polisi jambo ambalo
hakufanya.
Kamanda
MISIME amewaomba wananchi wenye taarifa na dereva huyo alipo wajulishe
katika kituo chochote cha Polisi ili aweze kukamatwa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment