Staa wa filamu Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amedaiwa kujiweka kwa Pedeshee
Chifu Kiumbe baada ya siku kadhaa zilizopita kumfuata na kumtaka
amsaidie katika project ya filamu yake .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya msanii huyo kupewa sapoti ikiwa ni
pamoja na gari la kushutia, mdada huyo amekuwa akijionesha kuwa pedeshee
huyo ni mtu wake.
“Alipopewa sapoti hiyo akaona ndiyo ajiweke kabisa bila kujua kuwa Chifu
Kiumbe alikuwa akimsaidia tu na wala hakuwa na wazo la kumtaka,” alidai
sosi huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya habari hizi kunaswa, mapaparazi wetu walimtafuta pedeshehe huyo
ambaye alisema: “Hata mimi nashangaa kusikia watu wakisema natoka na
yule dada, ukweli sijawahi kuwa mpenzi wake alikuja kuniomba msaada wa
project yake nikamsaidia hata gari nilimpatia lakini nimesikia eti
ananiita bebi kwenye mitandao ya kijamii, siyo kweli kabisa.”
Batuli naye anasemaje? Huyu hapa: “Mh! Watu wananisema mengi sana,
waache waseme, mimi naongea na Chifu kawaida tu, hata jana nilimfuata
anisaidie kama wasanii wengine.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment