Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Waandamanaji wa upinzani nchini Venezuela
Polisi nchini Venezuela wamekabiliana na waandamanaji wa upinzani katika barabara za mji mkuu wa Carcas ambao wanataka kuachiliwa huru kwa wanafunzi waliokamatwa wiki iliopita.
Polisi wa kukabiliana na ghasia walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya huku waandamanaji hao wakiwatupia mawe.
Awali maelfu ya wafuasi wa Rais Nicholas Maduro pia walishiriki katika maandamano ya kuwapinga waandamanaji hao katikati mwa mji mkuu wa Carcas.
Rais Maduro ameushtumu upinzani kwa kuzua fujo kwa lengo la kutaka kuipindua serikali yake.
Watu watatu waliuawa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya jumatano.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry ,ametoa taarifa akiitaka serikali ya bwana Maduro kuwaachilia huru wafungwa wote waliokuwa wakiandamana mbali na kuheshimu uhuru wa kujieleza.
>>>>>bbcswahili

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top