Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE), tawi la Dar es Salaam, kimemfukuza kazi
mhadhiri wa chuo hicho anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa
maadili ikiwamo kufanya ngono.
Mhadhiri
huyo ambaye jina halikutajwa alinaswa na kamera za kisasa za kurekodi
matukio za CCTV zilizofungwa kwenye vyumba vya madarasa ili kudhibiti
nidhamu, miongoni mwa wanafunzi na wahadhiri.
Kamera
hizo zimefungwa kwenye vyumba vya madarasa 20 ili kudhibiti vitendo vya
ngono baina ya walimu na wanafunzi, wizi wa mitihani na matendo mengine
yanayovunja sheria.
Hayo
yalibainishwa jana jijini na mkuu wa chuo hicho, Profesa Emanuel Mjema,
alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.
Profesa
Mjema, alisema, walifikia maamuzi ya kuweka kamera hizo za kisasa ndani
ya madarasa Aprili mwaka jana baada ya kujiridhisha na taarifa za
kuwapo matukio ya ukosefu wa maadili miongoni mwa wahadhiri ikiwa ni
pamoja na kutoa alama za juu kwa baadhi ya wanafunzi wa kike baada ya
vitendo vya ngono.
“Nilipoingia
chuoni hapa Januari mwaka jana, nilisikia kuwa kuna baadhi ya wahadhiri
wamekosa maadili, wanatoa alama za juu kwa wanafunzi wa kike kwa
masharti hata kama hawajafaulu kwa kiwango hicho. Nikaona vyema tuweke
vifaa hivyo ili kudhibiti vitendo hivyo,” alifafanua Profesa Mjema.
Alieleza
kuwa baada ya kuweka kamera hizo 20 kwa kila darasa kuwa na kamera
moja, walifanikiwa kumnasa mwalimu mmoja kwa kitendo cha kukiuka maadili
yake ya kazi na kumfukuza kazi.
Alisema
kuwa, kamera hizo pia, zinasaidia kuwadhibiti wanafunzi wenye tabia ya
kuiba mitihani, kwani mikakati iliyopo hata wakufunzi na wanafunzi
hawajui anayetunga mitihani ili mradi ipo ndani ya silabasi ya chuo.
Kamera
hizo zinadaiwa kuwa na uwezo wa kumvuta karibu mwanafunzi aliyeko
darasani na kujua anachokiandika, pia mhadhiri iwapo anachokifundisha ni
cha ukweli au anadanganya kwa hiyo zinatumiwa wakati wote kwenye
vipindi na mitihani.
Alisema,
chuo kimeajiri walinzi kwa ajili ya kuwadhibiti wanafunzi ambao wanavaa
nguo ambazo hazina maadili mazuri na pia hukagua vitambulisho
wanapofika getini, lengo likiwa ni kukifanya chuo hicho kubakia katika
heshima yake.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri, Mbene, alipongeza jitihada hizo zilizofanywa
na chuo hicho, huku akikemea vikali tabia inayofanywa na baadhi ya
wahadhiri hao, akiongeza kuwa, ni lazima mwanafunzi apewe madaraja ya
matokeo ya mitihani kutokana na ufaulu na uwezo wake.
Pia,
aliahidi kushughulikia suala la uvamizi wa eneo la chuo hicho pamoja na
maombi ya kuongezewa madarasa ikiwa ni pamoja na kupewa majengo ya
Wakala wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa (NFRA).
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment