Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 
STAA wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kubembeleza penzi kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.....

 
Nay wa Mitego na Nisha katika pozi la kimahaba enzi za penzi lao.
Mnyetishaji wetu alivujisha mawasiliano baina ya wawili hao waliowahi kuwa wapenzi kisha kumwagana ambapo yalionyesha kuwa Nisha analitamani upya penzi la staa huyo.

Mbali na mawasiliano ya ujumbe wa maandishi, chanzo hicho kilicho karibu na mastaa hao kilikwenda mbali zaidi kwa kuvujisha picha ambazo zilionesha Nisha akimtumia Nay huku akichombeza na meseji tofauti za kumtega.

 
Nay na Nisha katika pozi.
Baada ya kuzinasa meseji hizo ambazo chanzo kilidai kimeziiba kutoka katika moja ya simu ya mastaa hao, paparazi wetu aliingia mzigoni kuwasaka mastaa hao ili kujua kama wana mpango wa kurudiana.

Wa kwanza kupatikana alikuwa ni Nisha ambaye alisema: “Dah, ni kweli ninawasiliana na Nay kama rafiki wa kawaida tu.

“Nay ana demu wake na mimi nina bwana wangu.”

Kwa upande wa Nay wa Mitego alipata kigugumizi kidogo kulizungumzia hilo lakini akakiri kupata meseji hizo za mitego lakini akadai hakuna kinachoendelea kati yao.

-credit: ijumaa via gpl

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top