
Mgonjwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Naivasha
Wananchi wa Kenya wameshangazwa
na taarifa ya mwanamume mmoja aliyedhaniwa kuwa mfu kufufuka kutoka
katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali moja mjini Naivasha
umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu Nairobi.
Wafanyakazi wa hospitali hiyo
walipigwa na butwaa na hata kutoroka walipoona mwili wa mtu aliyedhaniwa
kufariki ukisonga na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba cha
kuhifadhia maiti.
Afisaa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo ya
wilaya, Dokta Joseph Mburu, alisema kuwa dawa iliyotumiwa kumtibu Mburu
hufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda ilimfanya muuguzi
kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Nusura Mburu awekwe kwenye jokovu la kuhifadhia maiti.
Jamaa za mwanamume huyo akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha maiti siku ya Alhamisi ili kujiandaa kwa mazishi , lakini baadaye mchana walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
Source:bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment