
Mkalimani
wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais
wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika
hospitali ya magonjwa ya ya akili. Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.
Wataalam wa
lugha ya ishara wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi
mbalimbali wakitoa hotuba zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson
Mandela wiki iliyopita.
Bwana Jantjie amesema aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia. Amesisitiza kuwa alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.
Chama tawala
cha African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana
Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za
nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa
ujuzi au maradhi yoyote.
Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.
Chanzo - BBC Swahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment