Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita kwamba kama
ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye atafurahi sana
kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.
" Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo.
"Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa
Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO
Rais akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi,"
amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.
Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia
aliyetaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri
wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri kutokana na ufisadi wa kutisha TAMISEMI.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment