
Marekani imepuuza pendekezo la kumsamehe Edrward Snowden ili akome kufichua taarifa zaidi
Jaji
wa mahakama katika jimbo moja nchini Marekani amesema kuwa mtindo wa
shirika la ujasusi la Marekani kukusanya data za kwenye simu za watu
binafsi ni kinyume na katiba ya nchi. Jaji
Richard Leon alisema kuwa tabia hiyo inaingilia taarifa za faragha za
watu na kuwa haistahili na pia wamarekani hawaishi kwa amani kwani simu
zao zote zinadukuliwa.
Mmoja wa
watu waliolishitaki shirika hilo kwa kufanya udukuzi wa simu za mkononi
za watu na kukusanya data nyingi ya watu binfasi Lary Klayman, amesema
kuwa shirika hilo sharti lijue kuwa linakwenda kinyume na sheria.
Larry
Klayman aliongea na BBC baada ya jaji Richard Leon, kuamua udukuzi wa
simu unaofanywa na shirika la ujasusi la Marekani unakiuka katiba ya
nchi kuhusiana na kukusanya taarifa kwa njia isiyofaa.
Baadhi ya
taarifa ambazo hukusanywa na shirika hilo ni namba za simu za watu,
nyakati walizopiga simu na tarehe walizopiga simu zao.
Sakata hili
lilifichuliwa na mtoro Edward Snowdon kuhusu tabia ya serikali ya
Marekani kufanyia simu za watu udukuzi katika juhudi zao za kutafuta
taarifa za kijasusi.
Jaji Leon alitoa agizo la muda la kuzuia shirika hilo kuendeleza udukuzi ingawa anasuburi serikali kukata rufaa.
Ikulu ya
White House ilipuuzilia mbali pendelezo kuwa Bwana Snowden ambaye
alikimbilia nchini Urusi baada ya kufichua taarifa hizo kupewa msamaha
ili aweze kukoma kuendelea kufichua taarifa hizo.
Chanzo - BBC SWahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment