TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUSITISHA
LESENI ZA USAFIRISHAJI KWA MABASI YANAYOMILIKIWA NA KAMPUNI
ZA OSAKA ROYAL CLASS, POLEPOLE CLASSIC NA BURHAN BUS SERVICES
Hivi
karibuni mabasi yanayomilikiwa na kampuni za Osaka Class, Polepole
Classic na Burhan Bus Services yalihusika katika ajali zilizotokea
katika maeneo na siku tofauti ambapo watu walipoteza maisha na wengine
wengi kujeruhiwa.
Kutokana na hali hiyo Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imechukua hatua kwa wahusika kama ifuatavyo:
1. Kampuni ya Osaka Royal Class
Mnamo tarehe 10/12/2013, Basi la Kampuni
ya Osaka Royal Class lenye namba ya usajili T819BYL lililokuwa
likiendeshwa na Bwana Emmanuel Semkamba kutokea Arusha kuelekea Dar es
Salaam, lilipata ajali maeneo ya Kirinjiko katika Wilaya ya Same Mkoani
Kirimanjaro. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watatu (03) na
majeruhi thelathini na watatu (33).
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa
kulimudu baada ya kupata hitilafu ya kiufundi kutokana na mwendo kasi.
Kwa
kuzingatia Kifungu Namba 15 cha Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba
22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma za Mwaka 2008,
Mamlaka imeamua kusitisha leseni za usafirishaji kwa mabasi
yanayomilikiwa na kampuni ya Osaka Royal Class yenye namba za usajili
T819BYL, T417 AAG, T852 AUL, T206 CJZ, T201 CJZ, T437 BJK na T852 AUL.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
2. Kampuni ya Polepole Classic
Mnamo tarehe 8/12/2013, Basi la Kampuni
ya Polepole Classic lenye namba za usajili T898BKN likiendeshwa na
Stephano Pangawazi kutokea Moshi kuelekea Babati, lilipata ajali maeneo
ya Kijiji cha Machangarawe katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watano(5) na majeruhi thelathini
na wawili (32).
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi
zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa
kuchukua tahadhari wakati akiendesha basi usiku kulikopelekea kuligonga
trekta lililokuwa likiendeshwa barabarani.
Kwa kuzingatia Kifungu Namba 15 cha
Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama
na Ubora wa Huduma za Mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha leseni za
usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na Kampuni ya Polepole Classic
katika njia ya Moshi-Babati yenye namba za usajili T898 BKN, T267AZL na
T212BLZ.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
3. Kampuni ya Burdani Bus Service
Mnamo tarehe 12/12/2013, basi lako lenye
namba za usajili T610ATR lililokuwa likiendeshwa na Bwana Ruta Kwadahel
likitokea Korogwe kuelekea Dar es Salaam, katika barabara ya Arusha-
Dar es Salaam lilipata ajali maeneo ya Kijiji cha Taula, Wilaya ya
Handeni, Mkoani Tanga. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 12 na
majeruhi 93.
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi
zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, uzembe wa dereva wa
basi hilo na kujaza abiria kupita kiasi.
Kwa kuzingatia Kifungu Namba 15 cha
Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama
na Ubora wa Huduma za Mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha leseni za
usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo yenye namba za
usajili T158BXG, T610ATR, T572BXJ, T994AGD, na T607ATR.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
Imetolewa na:
David Mziray
Meneja Mawasiliano
SUMATRA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment