Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akichangia hoja kwenye mjadala wa
kupitisha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2014/15, mjini
Dodoma jana. Picha na Edwin MjwahuziDar es Salaam/Dodoma.Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema ana shaka kama Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now), utafanikiwa kutokana na Kitengo cha Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo kilicho chini ya Ofisi ya Rais (PDB) kukosa meno.
Akichangia mjadala wa hoja ya Mapendekezo ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015, Lowassa alisema tatizo
kubwa linaloikabili nchi ni viongozi kushindwa kutekeleza mipango
mbalimbali ya maendeleo.
“Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo mengi lakini
hakuna utekelezaji,” alisema Lowassa wakati akichangia mjadala huo
uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu),
Stephen Wassira, wiki iliyopita.
Mbunge huyo wa Monduli (CCM), Lowassa ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje alisema itakuwa vigumu kwa
PDB kutekeleza wajibu wake wakati hakina meno ya kusimamia utekelezaji
wa mipango ya Serikali.
Kitengo cha PDB kinachoongozwa na Omar Issa
kiliundwa mwaka huu na kutengewa kiasi cha Sh29 bilioni na kulalamikiwa
na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika wakati wa kikao cha Bunge cha
Bajeti 2013/14.
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ni sehemu ya
jitihada za Serikali kuinua uchumi kutoka wa chini hadi kufikia wa kati
ifikapo mwaka 2025.
“Nataka mjiulize maswali machache. Je, hawa PDB wana meno?” alisema Lowassa na kuongeza:
“Tunazungumza lakini mjue kuwa `discipline’
(nidhamu) ya wenzetu wa Malaysia ni tofauti na hapa kwetu. Hapa kuna
uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua bila
kutekeleza.” Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge, Lowassa aliitaka
Serikali kuwa na mipango michache ambayo itakayoweza kuifuatilia kwa
ukaribu na kuitekeleza. Alipendekeza kuwa ajira, elimu na kuendeleza
reli kuwa vipaumbele muhimu.
“Kinatakiwa chombo ambacho kinaweza kufanya uamuzi
mgumu unaotekelezeka kwelikweli. Bila kuwavika joho la kufanya uamuzi
ili kuwarahisishia utekelezaji wa kazi yao na wakawa na ‘function’
itakuwa ni kazi bure. Ni uamuzi mzuri kuanzisha mpango huu lakini
msipoangalia itakuwa kazi bure. Lazima wawe na meno ya kuuma
mkishakubaliana mambo yafanyike.”
Kila mtu analalamika
Lowassa alisema sasa Tanzania imekuwa nchi ya kila mtu kulalamika, kuanzia viongozi hadi wananchi.
“Wananchi na viongozi wote wanalalamika
haiwezekani kukawa na jamii ya aina hii, lazima awepo mtu mmoja
anayefanya uamuzi na anayechukua hatua. Bila kuchukua hatua tutaendelea
kulalamikiana tu” alisema.
kwa habari kamili bofya hapa
kwa habari kamili bofya hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment