 |
Zoezi la
kuhamisha makaburi 40 kutoka katika eneo
la ujenzi wa kizuizi cha mpaka baina ya nchi ya Tanzania na Burundi ,katika eneo
la Nzaza kata ya Kabanga wilayani Ngara Mkoani Kagera limefanyika leo(Novemba
04,2013) na miili ya Ndugu pamoja na Jamaa kuzikwa upya kutoka eneo hilo....Picha na Mdau Shaabani Ndyamukama-Ngara.
|
 |
Diwani wa
kata ya Kabanga Bw Said Soud amesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa amani na
kwamba mabaki ya miili 36 ilikuwa imepatikana na kuchukuliwa na ndugu zao kwa
ajili ya mazishi na kwamba Wanafamilia wa marehemu hao wameonyesha ushirikiano
wa kutosha, licha ya kuwepo changamoto
za matumizi ya vifaa duni vya
kuchimbulia makabuli na kubeba miili ya ndugu zao.
|
 |
Katika zoezi hilo wananchi waliokuwa wamesusia
kuhamisha makaburi ya ndugu zao na kuzuia makampuni yanayofanya kazi ya ujenzi
wa kizuizi hicho sasa wameungana pamoja baada ya kukubali viwango vya fidia.
|
 |
Wakiongea na Waandishi wa Habari katika eneo hilo wananchi wamesema serikali imefanya jambo la maana
kuwapatia fidhia ya fedha za kuhamisha makaburi hayo na kuzikwa upya kwa ndugu
zao.
“Tumepata
wakati mugumu kwani miili mingine ilikuwa ni ya siku za hivi karibuni hivyo
kuogopa kuifumua na kuleta madhara wakati wa kuihamishia kwenye majeneza
mapya”.Alisema Niyonzima Marchades
|
Katika hatua
nyingine, Diwani wa Kata ya Kabanga Bw Said Soud amewataka wakazi wa kata ya
Kabanga kutoa ushirikiano katika zoezi la kujenga kizuizi hicho kupitia kampuni ya ujenzi ya Lukolo Co.LTD.
Post a Comment
Post a Comment