Mwanafunzi aliyekuwa akisubiri kufanya mtihani wa kidato cha nne unaotaraji kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika Manispaa ya Iringa akiwa amejinyonga usiku huu kuhofu mtihani wa kidato cha nne
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe ulioachwa na marehemu huyu
Hii ndo Barua ilioachwa na marehemu huyo…
Mwanafunzi aliyekuwa akisubiri kufanya mtihani wa kidato cha nne unaotaraji kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika Manispaa ya Iringa akiwa amejinyonga usiku huu kuhofu mtihani wa kidato cha nne
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe ulioachwa na marehemu huyu
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara hivyo kuamua kujiua ili kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.
Kwani alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana huyo ameuacha .
Chanzo: Teamtz.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment