NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, amemchambua mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kusema kuwa ni mchanga kwenye siasa hivyo hamuogopi.
Hatua hiyo ya Mwigulu imekuja baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Dk. Kitila kumshangaa mbunge huyo wa Iramba Magharibi, kuwa amejifanya kumwonea huruma katika kipindi hiki ambacho amevuliwa wadhifa wake wakati hapo awali alikuwa akimponda.
Kutokana na hali hiyo, Nchemba alimtupia vijembe, Dk. Mkumbo ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, na kusema kuwa hana hofu kutokana na lengo lake la kulitaka jimbo hilo.
"Nakwambia mwandishi,Kitila akipata hata nusu ya kura zangu ndani ya jimbo la Iramba(wilaya) nitaandika barua tume ya UCHAGUZI wampe Ubunge,Mimi najiamini sana kwasababu mkataba wa maendeleo unaoniunganisha na Wanairamba nimeutekeleza kwa asilimia 90 ndani ya muda wa miaka miwili tu,Muulize kwenye chaguzi za serikali za mitaa kijijini kwake nilimpiga kura kiasi gani?Kijijini kwake KITILA ndipo nilipooongoza kwa kura za Ubunge na hata kwa uchaguzi wa juzi wa serikali za mitaa"
Mwigulu, alisema ana uhakika wananchi wa jimbo hilo wanamwamini na wataendelea kumwamini kwani yeye ni mbunge wa kwanza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya jimbo hilo.
Nchemba alisema kwa kuwa Dk. Kitila ni mwanasiasa mchanga kwake, anapaswa kuendelea kukua kisiasa na ndiyo maana amekuwa mstari wa mbele kumtetea na kumuhurumia pale anapoonewa.
Alisema maneno ya Dk. Mkumbo, yanatokana na tofauti zao kisiasa, kichama na kimtazamo, lakini yeye kama mwanasiasa kijana, anapenda kuona vijana wenzake wakipiga hatua.
Hivi karibuni, Dk. Mkumbo alisema kwamba Mwigulu anapaswa kukaa mbali na kuacha kimbelembele cha kumsifia na kwamba atahakikisha analichukua jimbo la Iramba Magharibi.
“Mwigulu Nchemba amekuwa akinichafua, lakini tangu nivuliwe nafasi yangu ndani ya chama amejifanya kunisifu na kunihurumia.
“Kutokana na hali hiyo, namuonya na kumwambia mvua inyeshe jua liwake ni lazima nitamvaa katika uchaguzi wa Ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao,” alisema Dk. Kitila.
CHANZO:JF
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment