Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


KINACHOTOKEA CHADEMA ni Changamoto za ukuaji wa demokrasia...na ndio Chama kinapumua...bado naamini mbowe na zitto wanaweza kumaliza tofauti zao na wakatoka pamoja wakiwa imara zaidi Kama Chama kwa maslahi ya demokrasia ya ushindani nchini. Najua wanajuana kuliko tunavowajua sisi, TUWAPATIE nafasi. Naamini wanatambua hasara ya kusambaratisha upinzani nchini.


Kufukuzana kwenye Chama sio sifa Bali woga..kukabiliana kwenye Chama ndio sifa kuu isiyoepukika kwa Chama kinachokua na chenye uhai. Hakuna Chama kulichofukuzana na kuimarika.vyote vilivyofanya hivyo vilisinyaa..naamini vikao vya juu vya CHADEMA vitabatilisha maamuzi ya kamati kuu yake. Watambue kuwa CHADEMA ikifa Leo itachukua sio chini ya miaka10 kujenga up ya Imani ya umma kwa upinzani.


Hivyo watazame kwa mapana wakitambua kuwa hakuna Chama hai duniani ambacho HAKINA mapambano ya ndani( internal struggle), ndio uhai wa Chama, Chama kilichokufa hakiwezi kuwa na mapambano ya ndani, ndio maana siamini Kama kuwa na mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya Chama ni uhujumu au dhambi kwa Chama Bali ustawi.


Ndio maana ni wajibu wa Chama makini kiwe na mfumo wa kukabili migogoro ya ndani isipitilize kuhatarisha uhai lakn iwepo kwajili ya uhai aw Chama kwasababu isipokuwepo hakitakuwa Chama Bali magereza ya kisiasa. Hivyo Ndivyo nionavyo Mimi Kafulila.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top