THE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu
ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi
yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu
kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.
Baada
ya staa huyo wa filamu za ‘kikwetukwetu’ kuulizwa na kujibu hivyo
wikiendi iliyopita, alitundika picha nyingine kwenye ukurasa wake katika
mtandao wa kijamii wa BBM zikimuonesha akiwa nyumbani kwake,
Kijitonyama jijini Dar huku madhara ya mkorogo yakionekana waziwazi
kwenye mwili wake.
..Mapaja ya mrembo huyo.
Baadhi
ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine
kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo
vimemfanya apasuke kiasi hicho.Wema, baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi maduka yanayouza yafungwe.
Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment