Mbunge-Zitto Kabwe. |
CHADEMA na NCCR-Mageuzi tuna jumla ya madiwani 13 katika halmashauri ya Wilaya Uvinza. Ni mamlaka mpya inaanza tarehe 20 Julai, 2013.
CCM ina madiwani 8 tu, hivyo a clear majority kwa upinzani.CHADEMA ina madiwani 7,NCCR-Mageuzi 5 + Mbunge 1.
Leo (Julai 17,2013) sekretarieti za vyama vyetu zinakaa kuamua chama gani kati ya CHADEMA na NCCR-Mageuzi kitoe Mwenyekiti, makamu na wenyeviti wa Kamati.
Tukiendekeza tamaa zetu za kisiasa CCM watapita katikati yetu.
CCM wakichukua Halmashauri ya Uvinza yenye madiwani wengi wa upinzani itakuwa Ni usaliti mkubwa Kwa wananchi.
Nimewasihi viongozi wa vyama vyote 2 kuwa na hekima na kuzingatia matakwa ya wananchi waliotoa ridhaa mwaka 2010 na hivyo CHADEMAna NCCR-Mageuzi kuongoza Halmashauri ya Wilaya Uvinza.
Ni jaribio la demokrasia, Hekima na Maamuzi.
Source:-akaunti ya Zitto Facebook.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment