Baadhi ya mitandao tangu juzi imeandika kuwa muigizaji maarufu
Swahiliwood Rose Ndauka huenda ana mimba baada ya hivi karibuni kudaiwa
kuugua ghafla alipokuwa location, na presha kumpanda pamoja na
kichefuchefu wakati akishuti filamu yake mpya ya Jawabu na kupelekea
kuomba msaada baada ya kujisikia vibaya. Baada ya habari hizo kuenea
baadhi ya mashabiki wa muigizaji huyo mwenye kipaji cha kuigiza walituma
ujumbe SWP ili kumuuliza star huyo kama ni kweli anatarajia kupata
mtoto au lah. Hata hivyo Rose alipoulizwa na SWP alisema habari hizo sio
za kweli na hana mimba. "sio kweli na kilichoandikwa sijakiongea"
alijibu kwa ufupi actress huyo aliyejaaliwa mvuto.http://swahiliworldplanet.blogspot.com
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment