Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


MATUKIO, kauli na vitendo vya familia ya Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye ni mgonjwa mahututi, vimeanza kuashiria msiba kabla ya kutangazwa kwa kifo chake.
Sambamba na hayo, matamshi mbalimbali yaliyokwishatolewa na yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kisiasa wa ndani na nje ya Afrika Kusini na kw
a namna hiyo hiyo yakitolewa pia na watu wanaoheshimika duniani, yana mwelekeo wa kuwepo kwa msiba wa mzee Mandela ambaye amelazwa katika Hospitali ya Medi Clinic kwa siku ya 32 leo.

Ingawa Serikali ya Pretoria na baadhi ya wanafamilia wa mzee Mandela wamekuwa wakisisitiza kwa muda mrefu sasa kuwa bado yu mzima lakini mahututi kitandani, mparanganyiko ndani ya familia yake uliosababishwa na ugomvi wa makaburi ambao unadaiwa kuwa na mkono wa Serikali ya Pretoria, unaashiria kila dalili kuwa hataamka tena.


Ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu alipolazwa, familia yake imekuwa katika pilikapilika zilizozaa ugomvi kuhusu mahali atakapozikwa.

Wafuatiliaji wa mambo wamekuwa wakieleza kuwa hayakuwepo maandalizi ya mapema ya mahali pa kumzika Mandela, jambo ambalo limeiweka serikali na familia yake kwenye wakati mgumu kipindi hiki cha sintofahamu kuhusu hali ya afya yake.

Wanahabari wa mataifa mbalimbali waliopo Afrika Kusini, wachambuzi wa mambo na hata wananchi wengine wa kawaida, wamekuwa na imani kuwa, Serikali ya P
retoria haikuwa imejiandaa kwa msiba wa Mandela bali imezinduka usingizini sasa baada ya moyo wa Mandela kusimama kufanya kazi wakati akikimbizwa kwenda Hospitali ya Medi Clinic.

Imani hii kuwa mzee Mandela hataamka kutoka usingizini, pia imejengeka baada ya kupatikana kwa taarifa za Mandla Mandela, mjukuu mkubwa wa kiume wa familia ya Mandela kuingia eneo la makaburi ya familia nyakati za usiku na kufukua mabaki ya miili mitatu ya wanafamilia hiyo aliyokwenda kuizika ndani ya himaya yake ya kichifu ya Mvezo, kwa kile kinachodaiwa kujiandalia mazingira ya kuhodhi shughuli za mazishi na kaburi la mzee huyo, lengo likiwa kujinufaisha kiuchumi.

Zipo taarifa kuwa, baada ya hali ya Mandela kuwa tete, Serikali ya Pretoria ikiwa imekwishazinduka usingizini, iliamua kumtumia Makaziwe Mandela, binti mkubwa wa familia hiyo, kuandaa mazingira mazuri ya msiba na mazishi.

Taarifa zinaeleza kuwa hilo liliwezekana baada ya Makaziwe kufanikiwa kumdhibiti Mandla aliyelazimishwa na mahakama kurejesha mabaki ya miili ya watoto wa Mandela, ambayo yeye (Mandela) aliagiza azikwe pembeni ya makaburi yao.

Wakati imani hiyo ikiwa mioyoni mwa wengi, wadadisi wa mambo wamekuwa wakihoji ujumbe ulio ndani ya matamshi yaliyotolewa hivi karibuni ya mke wa Mandela, Graca Machel Mandela, ambaye amekuwa akimzungumzia mumewe kwa wakati uliopita.

Kauli za hivi karibuni za Graca alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa siku ya utamaduni na michezo ya Mandela huko Houghton Johannesburg, zilijielekeza kwenye kukumbuka, ambako alikuwa akitumia zaidi neno ‘tutamkumbuka’ na zinatafasiriwa kuwa zilikuwa zikimzungumzia mtu ambaye muda wake umekwishapita.

Pamoja na kauli hizo, agizo la Graca la kutaka maua na kadi za kumtakia kheri Mandela vipelekwe kwenye jumba lake la makumbusho, nalo linachukuliwa kulenga jambo lile lile kuwa sasa kilichobaki ni kumkumbuka.

Kwa waandishi wa habari wa mataifa mbalimbali walio nchini hapa wakifuatilia hali ya afya ya Mandela, wanaeleza kuwa siyo jambo la kawaida kwa Malkia wa Uingereza kutuma maombi ya kuhudhuria kifo cha mtu maarufu na anayeheshimika duniani wa aina ya Mandela iwapo bado kuna matumaini ya kuendelea kuwepo kwake.

Tayari Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza, alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akitoa ombi la kuhudhuria msiba wa Mandela atakapofariki.

Wakati huo huo, wataalamu wa tiba ya binadamu waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti nje ya uzio wa Hospitali ya Medi Clinic, Pretoria, kuhusu mwenendo wa afya ya Mandela, wamekuwa wakieleza kuwa tangu Mandela alipolazwa hajawahi kuzungumza.

Wakitoa maoni yao huku wakisisitiza kuwa yachukuliwe kuwa ni maoni binafsi kwa mujibu wa taaluma zao za kitabibu kwa sababu siyo wasemaji wa hospitali wala wa familia, walisema uwezekano wa Mandela kuamka katika usingizi aliolala sasa akipumua kwa nguvu ya mashine ni mdogo.

Mandela alikimbizwa hospitali Juni 8, baada ya kuanza kusumbuliwa na mapafu na tangu wakati huo, hajaelezwa kupata nafuu isipokuwa alilazimika kuwekewa mashine ya kumsaidia kupumua, jambo lililoashiria kuwa katika hali mbaya.

Wanatoa mfano kwa kueleza kuwa Serikali ya Pretoria, mara kadhaa imekwishaeleza kuwa hali ya mzee Mandela ni mbaya na Rais Jacob Zuma, alilazimika kuahirisha safari yake ya kikazi ya nchini Msumbuji baada ya kumjulia hali na kubaini kuwepo kwa jambo lisilokuwa sawa.

Maoni haya ya matabibu yanaungwa mkono na wanahabari wa mataifa mbalimbali waliopo Medi Clinic, Pretoria, ambao hata hivyo hawajafanikiwa kupenya na kufika alipo Mandela ili kujua hali yake, wanaoeleza kuwa kin
achofanywa sasa mamlaka za hapa ni kuandaa msiba kabla ya taarifa za kifo.

Ikiwa ni siku ya 32 leo tangu alipolazwa hospitalini, taarifa zinasema hali yake haijabadilika, kwamba bado ni mbaya lakini yuko imara.

                                                      Mtanzania

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top