
MAMA mzazi wa beki wa kati wa Chelsea, John Terry, Sue, amekutwa
akiwa amelewa chakari na kuuchapa usingizi katika siti ya nyuma ya
teksi aliyokodi baada ya kuzidiwa na pombe alizokunywa usiku kucha
katika baa moja jijini London.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 55, alipanda ndani
ya teksi hiyo saa 9 za alfariji akiwa ametoka kuponda raha na mkwewe,
mke wa Terry, Toni.
Kwenye teksi hiyo, bibi Sue alitangulia kupanda na
kwa sababu alichoka, aliamua kuangusha usingizi katika siti ya nyuma
akimsubiri Toni atoke ili warudi nyumbani.
Tukio hilo la ulevi wa mama huyo, limekuja siku
chache baada ya baba mzazi wa mwanasoka huyo kupandishwa kizimbani kwa
tuhuma za ubaguzi.
Na mwanaspoti
Na mwanaspoti
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment