Ile habari ya juzi ya binti mwenye elimu ya darasa la saba anayeuza dawa katika famasia, haikutosha, ipo nyingine ya kutoa huduma za afya katika zahanati bubu, katika kiwango cha utaalamu wa mabingwa (specialist), kwa asiye na sifa hata ya ngazi moja kabla ya hiyo.
Tunao mitaani. Wapo. Na tunafahamu. Ila kama kawaida, twajitia hamnazo, hayatuhusu, mwache atafute mkate wake. Shauri lao wanaokwenda huko.
Kila uchao watu ni kulalamika kuhusu huduma mbovu za afya, lakini papo hapo ni watu hao hao walio mstari wa mbele kufumbia macho na kutokuchukua hatua kudadisi kuhusu uhalali wa huduma wanayoipata. Labda ni elimu duni kwa ujumla na elimu duni katika suala husika.
Basi, tuendelee kuhalalisha makosa ya wengine kwa kuwa wengine walikosea, hasara na faida ni kwetu sisi wananchi, kama si wewe basi kwa ndugu, jamaa, rafiki ama jirani yako.
ITV, Dar es Salaam — Kijana mmoja amekutwa akitoa huduma za tiba zinazotolewa na madaktari mabingwa wa magonjwa ya wanawake katika zahanati bubu maarufu kwa jina la kwa Dokta Kondoliza eneo la Mji mpya Majohe.
ANGALIA VIDEO HAPO CHINI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment