Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

                        
Kulikuwa na kosta ina ovateki kwenye matuta, halafu mbele ya kosta kulikuwa na tax aina ya colora, upande wa kulia kulikuwa na pikpiki inatoka mjini kwenda kange, kwa hiyo huyu wa kosta aliyo ovateki akakutana na pikpiki alipotaka kurudi upande wake akawa amemgonga mwenye tax kwa nyuma. Pikipiki haitamaniki yani nyang'anyanga'a!, Tax kwa nyuma ni
nyang'anyang'a pia, Kosta kwa mbele ni balaa japo haijavunjika vioo. Dereva wa bodaboda amechanika kichwani na ametokwa na damu nyingi sana kichwani na masikioni, alikuwa kavaa kofia, pia amevunjika mguu kwenye paja ambao sidhani kama atapona maana ulivimba fasta!. Baada ya dakika tano pikipiki aina ya bodaboda iliyokuwa na abiria mmoja ilianguka umbali wa hatua 30 kutoka kwenye eneo la tukio yani ajali nyengine tena!, abiria ameumia sehemu ya miguu na pikipiki imeharibika japo si sana. Ntaendelea kuwajulishana kitakachoendelea wasomaji wangu..

IMERIPOTIWA KWA MASAI NYOTAMBOFU BLOG NA  David Mtengile

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top