Umati wa watanzania waliojitokeza kuuaga mwili wa Mangwea jijini Dar es Salaam leo
WAKATI msarafa wa mwili wa aliyekuwa masanii wa muziki wa kizazi
kipya,nchini Tanzanani marehemu Albert Mangwea ukielekea mjini Morogoro
kwa mazishi, Rais wa Shirikisho la Muziki wa Kizazi kipya Tanzania (TMF)
Addo November Mwasongo amezishambulia vyombo vya habari na kudai kwamba
ziliandika vibaya taarifa za kifo cha msanii huyo.
Akizungumza wakati wa kusoma lisala ya TMF katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Mwasongo alisema kwamba, ”Tunalaani
vikali vyombo vya habari vilivyokuwa vinaendelea kutoa habari ya
kumchafua marehemu,tunasema huo si uungwana wala mila za kitanzania
kumsema vibaya mtu ambaye hawezi kujibu(marehemu)tena kwa kutunga wakati
hawajaiona ripoti ya daktari jambo hili halikubaliki hata siku moja”:.
"TMF ilipokea taarifa za kifo cha Mangwea kwa huzuni mkubwa sana na
tukaungana na familia ya marehemu pamoja na watanzania wengine wakati
huu wa msiba, Kamati hii pia inampa pole sana mwanamuziki Mgaza Pembe (M
TO THE P) na kuwaomba watanzania tuzidi kumwombea mwanamuziki huyu mola
amjalie afya njema na yenye baraka".
Mwasongo alisema kwamba TMF imewashukuru watanzania kwa kujitokeza
kwa wingi na kuonyesha ushirikiano wao wakati wa msiba wa msanii huyo na
kutoa heshima zao za mwisho wakati wa kuuaga mwili wakeFacebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment