Mwanamuziki
aliyevumbua staili ya muziki ya TAKEU (Tanzania Kenya Uganda),
Mtanzania Lukas Mkenda aka Mr Nice amepoteza mkataba wake na kampuni ya
kurekodi muziki ya nchini Kenya, kwa kile kilichoelezwa na kampuni hiyo
kuwa ni tabia ya Mr Nice ya uvivu, ulevi, asiyeaminika na asiye na
ushirikiano.
Zaidi
ya maandishi yaliyoandikwa na GrandPa Records kwenye ukurasa wao wa
Facebook, pia wamezungumzia suala hilo walipohojiwa na kituo cha EA
Radio ambapo wamesema Mr Nice amesema ataendelea kubaki mjini Nairobi
nchini Kenya akitafuta kujiweka sawa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment