Moto
uliowashwa na baadhi ya watu wakifunga barabara baada ya kutawanywa na
Polisi kwa mabomu ya machozi katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini
hapa, barabara Iiliyopo eneo la Kaloleni. (Picha zote na Ferdinand
Shayo)
Moto ukiwaka katikati ya barabara wakati wa vurugu zilizotokea katika viwanja vya SOWETO mjini Arusha.
Wanafunzi
wa shule wakijiziba na nguo na kunawa uso baada ya kudhuriwa na mabomu
ya machozi yaliyopigwa leo na Polisi waliokuwa wakitawanya maelfu ya
watu waliokuwa kwenye mkutano katika viwanja vya SOWETO.
Baadhi ya
watu wakifunga barabara baada ya kutawanywa na Polisi kwa mabomu ya
machozi katika viwanja vya SOWETO vilivyopo jijini hapa, Barabara Kuu
inayopitisha magari ya mikoani eneo la Kimahama.
ARUSHA, Tanzania
MBUNGE wa
Mbulu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Mustafa Akoonay, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu,
viongozi wengine wa Chadema na wafuasi kadhaa wa chama hicho
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Arusha kwa mahojiano kufuatia
vurugu zilizoibuka katika mkutano wa hadhara.
Akizungumza
na Habari Mseto Blog kutoka jijini Arusha, Kamanda wa Polisi mkoa huo,
Liberatus Sabas alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao waandamizi wa
Chadema na wafuasi wa chama hicho muda mfupi baada ya mkutano wa dharura
wa chama hicho katika uwanjwa wa Soweto.
Jeshi la
Polisi lilivunja mkutano huo kwa kutumia gesi ya machozi yaliyorindima
kwa zaidi ya saa mbili kutawanya wafuasi wa chama hicho uwanjani hapo,
kutokana viongozi hao kutumia nafasi ya maombolezo kuendesha mkutano
hadhara ambao haukuwa na kibali.
Watu
kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha katika tafrani hiyo, huku wengine
wakijeruhiwa na kufikishwa hospitali mbalimbali jijini humo, ikiwemo
Hospitali ya Seliani kwa matibabu baada ya kuumizwa na askari, huku
wengine wakipata mshtuko iliyosababishwa na mlipuko wa mabomu ya
machozi.
Wakiwa
ndani ya magari madogo, askari polisi walilipua mabomu hayo maeneo
mbalimbali ya jiji la Arusha hali iliyowalazimu wafanyabiashara jijini
humo kufunga biashara zao na kukimbia wakihofia kuvamiwa na wakazi
waliokuwa wakikimbia hovyo kunusuru maisha yao.
Hali ya
usafiri iligeuka adha nyingine kwa wakazi wa jiji la Arusha, baada ya
daladala kushindwa kutoa huduma hiyo, zikihofia mabomu yaliyokuwa
yakirushwa na askari, huku barabara zikifungwa baada ya wafuasi wa
CHADEMA kuchoma matairi barabarani.
Tafrani
hiyo kwa namna moja iliwaathiri hata wanahabari, ambao walijikuta
wakipata adha ya ulipuliwaji wa mabomu hayo na kulazimika kujificha
katika magofu ya nyumba za AICC zilizoko karibu na uwanja wa Soweto kwa
zaidi ya masaa mawili.
Aidha,
mapema Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, alikiri kuwa uchunguzi wa
haraka umebaini kuwa bomu lililotumika kulipua katika mkutano wa Chadema
juzi limetengezwa China, na aina hiyo ya mabomu yanamilikiwa na vyombo
vya dola, hasa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment