Mtandao wa Wavuti
unaripoti taarifa ya Neville Meena kuwa ingawa ni kweli kuna ajali ya
boti iliyotokea, mwanamuziki Saida karoli hakuwa mmoja wa waliokuwemo
kwenye boti hiyo na yuko hai!
Taarifa hiyo imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa
Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam: “Nimetafuta namba yake
ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa
Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli…” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “…ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria, na kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.”
Nayo Upland FM radio, Kwa kupitia Facebook page yake, imekanusha taarifa za kufariki Saida karoli na kusema msanii huyo ni mzima wa Afya. “TAARIFA: Kumezuka habari zisizo rasmi juu ya mwanamuziki SAIDA KALORI. Tunaomba kuthibitisha kwa Mwanamuziku huyo ni MZIMA wa afya kabisa. Usidanganywe na uzushi wowote. ASANTE.” imesema taarifa hiyo ya Upland FM

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment